Skip to main content

Farisi (kundinyota) YaliyomoMahali pakeJinaNyotaTanbihiMarejeoMarejeoUrambazajiThe Constellationsonline hapa kwenye archive.orgkuihariri na kuongeza habari

Mbegu za sayansiAstronomiaKundinyota


KilatiniKiingerezajinakundinyotaangakaskaziNjia Nyeupemitholojia ya KigirikiMara Mke wa KurusiKondooAriesNg`ombeWagiriki wa Kalemitholojia ya KigirikiAndromedaZeusDanaëMedusaKlaudio PtolemaioUmoja wa Kimataifa wa AstronomiaUKIAMrifakimwangaza unaoonekanamiakanuruRasi Medusaen:Algolmwangaza unaoonekananyota badilifuJenga Wikipedia ya KiswahiliWikimedia Community User Group Tanzania












Farisi (kundinyota)




Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru






Jump to navigation
Jump to search




Nyota za Farisi (Perseus) katika sehemu yao ya angani




Ramani ya kundinyota Farisi (Perseus) jinsi inavyoonekana kwa mtazamaji kwenye nusutufe ya kaskazini ya Dunia




Nyota za kundinyota Farisi (Perseus) jinsi alivyochorwa miaka 200 iliyopita pale Ulaya



Farisi (kwa Kilatini na Kiingereza Perseus) [1]. ni jina la kundinyota kwenye angakaskazi ya dunia.




Yaliyomo





  • 1 Mahali pake


  • 2 Jina


  • 3 Nyota


  • 4 Tanbihi


  • 5 Marejeo


  • 6 Marejeo



Mahali pake


Farisi linapitiwa na Njia Nyeupe. Lipo jirani na makundinyota mengine yenye majina kutokana na mitholojia ya Kigiriki kama vile Mara ( Andromeda) na Mke wa Kurusi (Cassiopeia), pia na makundinyota ya zodiaki Kondoo (Aries au Hamali) na Ng`ombe (Taurus).


Jina


Farisi lilijulikana kwa jina hili kwa miaka mingi kati ya mabaharia Waswahili waliotumia nyota kutafuta njia baharini wakati wa usiku.[2]


Jina la Farisi ni tafsiri ya jina lake la Kigiriki Περσεύς_Perseus na .Wagiriki wa Kale walitumia jina hili kwa kumtaja mtu kutoka “Persia” au “Fars” ilivyoitwa na Waarabu wasiojua herufi “P” na hapo Waswahili walipokea jina.


Katika mitholojia ya Kigiriki Farisi alikuwa shujaa aliyeua dubwana Ketusi na kumwokoa Andromeda. Baadaye wote pamoja na wazazi wa Andromeda mfalme Kifausi na malkia Cassiopeia waliinuliwa angani kama nyota [3]. Farisi alikuwa mwana wa ungu mkuu Zeus na Danaë. Aliwahi kumshinda dubwana Medusa aliyeweza kubadilisha kila kiumbe kuwa jiwe kwa kumwangalia tu lakini Farisi alikata kichwa chake. Baadaye alimwokoa Andromeda aliyefungwa kwa nyororo kwa mwamba kwenye ufuko wa bahari ili atolewe sadaka kwa Kestusi.




Farisi ni kati ya kundinyota zilizotajwa tayari na Klaudio Ptolemaio katika karne ya 2 BK kwa jina Kassiopeia. Iko pia katika orodha ya makundinyota 88 ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia [4] kwa jina la Perseus. Kifupi chake rasmi kufuatana na UKIA ni 'Per'.[5]


Nyota


Nyota angavu zaidi ni α Alfa Persei au Mrifaki yenye mwangaza unaoonekana wa 1.79 ikiwa umbali wa miakanuru 510.
Uangavu wake unafuatwa na β Beta Persei iliyoitwa Rasi Medusa (en:Algol) na mabaharia Waswahili. Ina mwangaza unaoonekana wa 2.12 ikiwa umbali wa miakanuru 90 kutoka Dunia. Hii ni nyota badilifu.











































































Jina la
(Bayer)

Namba ya
Flamsteed

Jina
(Ukia)


Mwangaza
unaoonekana


Umbali
(miaka nuru)

Aina ya spektra
α
33

Mrifaki (Mirfak)
1,79m592
F5 Ib
β
26

Rasi Madusa (Algol)
2,12 bis 3,39m93
B8 V
ζ
44
Menkib
2,9mca. 1000
B1 Ib
ε
45

2,90m538
B0.5 V
γ
23

2,91m256
G8 III
δ
39

3,01
528
B5 III
ρ
25
Gorgonea
3,2 bis 4,1m325
M3 III
η
15
Miram
3,77m1331
K3 Ib
ν
41

3,77m557
F5 II
κ
27
Misam
3,79m112
K0 III
ο
38
Atik
3,84m1476
B1 III

Tanbihi



  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Perseus" katika lugha ya Kilatini ni " Ceti " na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Ceti, nk.


  2. ling. Knappert 1993


  3. ling. Allen, Star-Names and their Meanings uk, 117


  4. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017


  5. Russell, Henry Norris (1922). "The New International Symbols for the Constellations". Popular Astronomy 30: 469–71.

Marejeo


Marejeo


  • Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 75 ff (online hapa kwenye archive.org)

  • Jan Knappert, 1993: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331




Science-symbol-2.svg
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Farisi (kundinyota) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Astrowiki.PNG


Mradi wa Astronomia

Makala hii imewahi kukaguliwa na kuboreshwa kwenye warsha ya pamoja ya Jenga Wikipedia ya Kiswahili, Wikimedia Community User Group Tanzania na ASSAT. Imepewa hali ya ulinzi. Tunaomba mapendekezo yote ya usahihisho na nyongeza zipelekwe kwanza kwenye ukurasa wa majadiliano











Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Farisi_(kundinyota)&oldid=1071830"













Urambazaji


























(RLQ=window.RLQ||[]).push(function()mw.config.set("wgPageParseReport":"limitreport":"cputime":"0.100","walltime":"0.123","ppvisitednodes":"value":557,"limit":1000000,"ppgeneratednodes":"value":0,"limit":1500000,"postexpandincludesize":"value":2771,"limit":2097152,"templateargumentsize":"value":815,"limit":2097152,"expansiondepth":"value":12,"limit":40,"expensivefunctioncount":"value":0,"limit":500,"unstrip-depth":"value":0,"limit":20,"unstrip-size":"value":1970,"limit":5000000,"entityaccesscount":"value":0,"limit":400,"timingprofile":["100.00% 49.009 1 -total"," 83.08% 40.715 1 Kigezo:Cite_journal"," 61.60% 30.192 1 Kigezo:Citation/core"," 7.15% 3.506 1 Kigezo:Mbegu-sayansi"," 5.33% 2.610 1 Kigezo:Citation/make_link"," 4.55% 2.231 1 Kigezo:Wikinyota"],"cachereport":"origin":"mw1271","timestamp":"20190918235155","ttl":2592000,"transientcontent":false););"@context":"https://schema.org","@type":"Article","name":"Farisi (kundinyota)","url":"https://sw.wikipedia.org/wiki/Farisi_(kundinyota)","sameAs":"http://www.wikidata.org/entity/Q10511","mainEntity":"http://www.wikidata.org/entity/Q10511","author":"@type":"Organization","name":"Uchangiaji katika miradi ya Wikimedia","publisher":"@type":"Organization","name":"Wikimedia Foundation, Inc.","logo":"@type":"ImageObject","url":"https://www.wikimedia.org/static/images/wmf-hor-googpub.png","datePublished":"2017-08-17T04:43:58Z","dateModified":"2019-07-20T09:21:24Z","image":"https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/1/1f/Farisi_Perseus.png"(RLQ=window.RLQ||[]).push(function()mw.config.set("wgBackendResponseTime":162,"wgHostname":"mw1328"););

Popular posts from this blog

Tamil (spriik) Luke uk diar | Nawigatjuun

Align equal signs while including text over equalitiesAMS align: left aligned text/math plus multicolumn alignmentMultiple alignmentsAligning equations in multiple placesNumbering and aligning an equation with multiple columnsHow to align one equation with another multline equationUsing \ in environments inside the begintabularxNumber equations and preserving alignment of equal signsHow can I align equations to the left and to the right?Double equation alignment problem within align enviromentAligned within align: Why are they right-aligned?

Where does the image of a data connector as a sharp metal spike originate from?Where does the concept of infected people turning into zombies only after death originate from?Where does the motif of a reanimated human head originate?Where did the notion that Dragons could speak originate?Where does the archetypal image of the 'Grey' alien come from?Where did the suffix '-Man' originate?Where does the notion of being injured or killed by an illusion originate?Where did the term “sophont” originate?Where does the trope of magic spells being driven by advanced technology originate from?Where did the term “the living impaired” originate?